Wednesday, July 31, 2013

Zimbabwe kuamua kati ya Mugabe, Tsvangirai leo

Harare. Wazimbabwe leo wanapiga kura kumchagua Rais na wabunge watakaoliongoza taifa hilo kwa miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo, Rais anayemaliza muda wake, Robert Mugabe anatetea kiti chake akichuana na mpinzani wake wa siku nyingi, Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai. Uchaguzi huo unafanyika huku Mugabe ambaye kupitia chama chake cha Zanu-PF akiwa ametawala kwa miaka 33, akipewa nafasi kubwa ya kumshinda Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC).

Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc), Bernard Membe alisema ana taarifa kuwa orodha ya majina ya wapiga kura haijawekwa wazi tangu juzi, ikiwa ni siku mbili kabla ya uchaguzi wa leo.

Alisema orodha ya wapiga kura siyo nyaraka za siri hivyo zilipaswa kutolewa mapema ili kila mpigakura aone jina lake.

“Orodha inatakiwa itolewe ili watu waione na kuhakiki majina yao, pia kujua vituo wanavyotakiwa kupigia kura,” Membe alikaririwa na BBC Focus on Africa akisema.


Tayari MDC kimetishia kwenda mahakamani kutokana na ucheleweshaji huo unaoweza kutia doa uchaguzi. Katibu Mkuu wa MDC, Tendai Biti alisema chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (Zec) ili kupata uhakika wa orodha hiyo. Uchaguzi wa leo huenda ukamaliza muda wa Serikali ya mseto baina ya Zanu-PF na MDC.

Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Alilazimika kuingia kwenye Serikali ya mseto baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2009 kutokana na shinikizo la Sadc ili kumaliza mzozo wa kisiasa uliokuwapo nchini humo.

Polisi 10,000

Ili kudhibiti usalama katika uchaguzi huo, zaidi ya polisi 10,000 wamesambazwa kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura. Redio ya Serikali ilitangaza jana jijini Harare kuwa polisi zaidi wamepelekwa Jimbo la Midlands wakiwa na silaha kadhaa zikiwamo bunduki na mabomu ya machozi. Pia ulinzi umeimarishwa katika maeneo ya katikati ya Harare, Highfield na Mbare.

Wafuasi wa Tsvangirai wameanza kushangilia katika maeneo ya wilaya mbalimbali hata kabla ya kupiga kura huku wengine wakiimba kwa kukumbuka ghasia za mwaka 2008, zilizosababisha wafuasi zaidi ya 200 wa MDC kuuawa

Pamoja na kura za maoni, ni vigumu kubashiri kama Tsvangirai (61) anayewania urais kwa mara ya tatu atamwangusha Mugabe (89).

Kila upande unajinasibu kupata ushindi na kwa hali ilivyo, ni wazi kuwa yeyote anaweza kuibuka mshindi na kupewa ridhaa ya kuwaongoza Wazimbabwe milioni 13. Waangalizi 500 wa kimataifa na 7,000 wa nchi hiyo, wamesema wana imani kuwa matokeo yatatangazwa ndani ya siku tano au chini ya hapo.

Kasoro zajitokeza

Zaidi ya polisi 63,000 na watumishi wa Serikali waliruhusiwa kupiga kura wiki mbili kabla. Hata hivyo, theluthi walishindwa kutokana na karatasi za kura kutofika vituoni kwa wakati.Pia Idadi iliyotajwa ya watu milioni 6.3 waliojiandikisha kupiga kura, imeanza kupigiwa kelele na MDC ikisema ni ndogo na kwamba inaweza kuwa kubwa zaidi ya hapo.

KANUNI ZA BUNGE:PINDA HAKUKOSEA

SIKU moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kueleza kusudio lao la kumshtaki Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kwa madai ya kuvunja katiba ya nchi Ibara ya 13 (1), wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma, Juni 19 mwaka huu, sakata hilo sasa limezidi kuchukua sura mpya.

Hali hiyo inatokana na Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM) kudai kuwa, hakubaliani na hauoni uhalali wowote wa LHRC kumfikisha mahakamani Bw. Pinda ambaye analindwa na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu ya mwaka 1988 pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100.
 Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia, alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama weweukijifa nyajeur iutapigwatu.
“Na miminase mam uwapige tukwasab abu hakunana mnanyin ginemaa natumechoka ”,alise maBw. PindaambapoB w.Sungus iaaliong eza kuwa ,kau li hiyoni kin yumech aK atiba , S heriazanchi namising iya HakizaBinad am u.
Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
 
Chanzo ( majira - Eckland Mwaffisi )

Mahakimu wenye shahada waanza kazi rasmi Mahakama za Mwanzo

Mahakama 290 kati ya 300 wenye elimu ya shahada, wamesambazwa katika Mahakama za Mwanzo nchini na wameanza kazi.

Hayo yalielezwa jana na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ignas Kitusi, wakati akizungumza na NIPASHE, juu ya uwepo wa sheria ya kuwawezesha Mahakimu hao kufanya kazi katika Mahakama hizo.

Alisema Mahakimu hao waliajiriwa mwanzoni mwa mwaka jana na walipelekwa kwenye mafunzo ya uhakimu kwa wiki moja katika chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto mkoani Tanga.

Alisema baada ya kuhitimu walisambazwa kwenye Mahakama mbalimbali nchini na walikuwa wanajifunza kazi kutokana na kutokuwepo kwa sheria ya kuwaruhusu kufanyakazi kwenye Mahakama hizo.

“Kazi ya uhakimu ni lazima mtu ajifunze, walikwenda kwenye vituo vya kazi kujifunza kazi na mwezi Aprili, mwaka huu, sheria ilipitishwa na kuwawezesha kufanya kazi…kabla ya hapo hawakuwahi kuamua kesi yoyote,” alisema.

Kitusi alisema kati yao 10 walihama na kwenda kwenye maeneo mengine ya utumishi wa umma.
Aidha, NIPASHE ilivyotaka kujua iwapo Mawakili wataanza kufanya kazi katika mahakama hizo, alisema elimu ya Hakimu haibadili hadhi ya Mahakama hivyo mawakili hawatatumika katika mahakama hizo.

Wakati wa kikao cha Bunge, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, akiwasilisha Mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2012/13, alisema mafunzo ya awali (Induction Course) kwa ajili ya Mahakimu Wakazi wapya 290 waliokuwa wameajiriwa kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo sehemu mbalimbali nchini yameshafanyika.

CHANZO ( NIPASHE - Salome Kitomary )

SERIKALI TATU NI KICHEKESHO - BARONGO

ALIYEKUWA Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Kapteni mstaafu, John Barongo amesema mapendekezo ya kubadilisha Muungano uwe wa Serikali tatu ni kichekesho hasa kwa kipindi hiki ambapo Afrika inafikiria kuwa na serikali moja.
 
Kapteni Barongo aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu rasimu ya Katiba Mpya na maoni mbalimbali yanayotolewa kuhusu muundo wa Katiba Mpya.Kapteni Balongo alisema, wazo la kuwepo kwa serikali tatu ni la baadhi ya viongozi wachache wanaotaka madaraka huku wengine wakizungumzia kuundwa kwa Katiba ya Tanganyika ili wapate uongozi badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.

Pamoja na hilo, Kapteni Balongo alikiri kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una matatizo na kusema kuwa hizo ni changamoto ambazo zinahitaji ufumbuzi wa pamoja na si kuwa na serikali tatu.Alisema, huko nyuma kuna baadhi ya nchi zilijaribu kuwa na muundo wa serikali tatu na kushindwa kuziendeleza huku akitolea mfano wa nchi ya Egypt na Syria ambazo ziliwahi kuunda Shirikisho la Syria (United Arab Republic) ambapo mwezi Septemba mwaka 1961 Mkuu wa Majeshi wa Syria alijiondoa katika shirikisho hilo na ukawa mwisho wa muungano huo.

"Nchi nyingine ni Mali na Senegal ambapo wao waliunda Mali Federation wakati huo Mali ikiitwa French Sudan, akachaguliwa Modibo Keita akawa Rais wa serikali hizo tatu na matokeo yake Rais wa Senegal wakati huo Leopold Sedar Senghor alijiondoa na ukawa mwisho wa shiririkisho hilo,"alisema Kapteni Barongo

Alisema kuwa, Watanzania wanatakiwa wajifunze kutoka katika nchi hizo kwani kuwepo na serikali hizo ni mzigo kwa wananchi kuhudumia marais wa serikali tatu hasa kwa wakati huu ambapo uchumi wa nchi si mzuri.Alisema kuwa, ni bora nchi ikabaki na serikali mbili kama ilivyo sasa na kisha kutatua mambo yanayokwamisha Muungano kuliko kuruhusu tatu ambazo zinaweza kuongezeka na kuwa nne kutokana na mapendekezo ya watu.

Hata hivyo, alitaka suala la ardhi lisiwe sehemu ya Muungano kwa sababu Wazanzibar wengi wanakuja Tanganyika na kujenga ambapo kwa Watanganyika inakuwa vigumu kupata ardhi Zanzibar.Akizungumzia mchakato wa Katiba mpya alisema, hakuna ulazima wa nchi ikawa na Katiba Mpya ifikapo mwaka 2015 na badala yake yaangaliwe mapungufu yaliyopo katika katiba ya sasa na kufanyiwa marekebisho.

"Mapungufu katika katiba ya sasa yapo ila kinachotakiwa ni kubainisha mapungufu hayo na kuyafanyia kazi na si kuiga nchi za jirani kama Kenya walivyobadili katiba yao, nadhani tungekuwa na katiba nzuri zaidi miaka 10 kutoka sasa,"alisema.

Katika hatua nyingine, Kapteni Barongo amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamia, amani, mshikamano na kupambana na ufisadi wa kila aina,kuwahudumia wananchi katika kupata haki zao na kuwakataa viongozi wanaotumia vitu hivyo kwa masilahi yao.

Alisema kuwa, wananchi wanajua nani anayefaa kuongoza nchi na kwamba Rais wa nchi hii anaweza kutoka chama chochote isipokuwa rais bora anatokea CCM.

Alisema kuwa, viongozi wa CCM lazima wabadilike na kuachana na kuongoza kwa mazoea ikiwa ni pamoja na kufahamu aina ya rais anayetakiwa kusimama mwaka 2015 asiyekuwa wa kununua watu bali wananchi wampende wenyewe.
 
Chanjo (majira - Rehema Mohamed )

Tuesday, July 30, 2013

Waziri afunga tena machinjio ya Ukonga

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk.Terezya Huvisa, ametangaza kuyafunga machinjio ya Ukonga Mazizini yaliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kutokana na kuendesha shughuli zake katika mazingira machafu yanayohatarisha afya za walaji wa nyama.
 Dk. Huvisa amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku 10 tangu atangaze kuwa ameshindwa kuzichukulia hatua Manispaa za Jiji la Dar es Salaam zilizoshindwa kusimamia usafi katika maeneo yao.
 Kauli ya kushindwa kuzichukulia hatua manispaa hizo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni ya usafi wa miji na majiji, kabla ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, kuanza ziara hiyo Julai 21 na 22, mwaka huu.
 Hii ni mara ya pili kwa machinjio hayo kufungwa na mamlaka za serikali katika kipindi cha mwaka huu, mara ya kwanza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc), liliyafunga kwa sababu kama hizo lakini siku nne baadaye yaliendelea na shughuli zake kama kawaida.
 Hatua ya machinjio hayo kuruhusiwa kuendelea na uchinjaji siku chache tu baada ya kufungwa na Nemc kulizua maswali mengi kwa wananchi wa kata ya Ukonga ambao walilitupia lawama baraza hilo kwamba huenda baadhi ya maofisa wake walipewa ‘kitu kidogo’ na kulegeza masharti.
 Akizungumza na wananchi wa Ukonga jana majira ya saa 3:30 asubuhi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika machinjio hayo, Waziri Huviza alisema anayafunga kutokana na kuendesha shughuli zake katika mazingira machafu.
 Alisema sababu nyingine ni kwamba machinjio hayo ambayo yameanza kuendesha shughuli zake tangu mwaka 1972, katika kipindi chote yamekuwa yakiendesha kazi zake bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Nemc kama sheria zinavyoelekeza. Waziri Huvisa aliwaagiza maofisa wa Nemc, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mazingira wa baraza hilo, Robert Mtakamalenga, kuandika barua haraka ya kusimamisha shughuli za uchinjaji katika machinjio hayo na kuiwasilisha kwa wamiliki wake jana.
 Alisema athari ambazo zitakuwa zimepatikana kwa wananchi kutokana na miundombinu mibovu ya mifereji ya kupitishia maji machafu uliopita karibu na makazi ya watu wamiliki wa machinjio hayo watawajibika kulipa gharama kwa waathirika.
 Akisoma taarifa kwa niaba ya wananchi wa kata ya Ukonga wanaoathirika kutokana na uchafu wa machinjio hayo, Bennett Bagonza, alisema hawana imani Nemc na Manispaa ya Ilala ambayo viongozi wake kila wanapoelezwa suala la uchafu katika machinjio hayo wamekuwa wakipuzia.
 
 
CHANZO ( NIPASHE - Thobias Mwanakatwe )

LHRC wapanga kumshtaki Pinda

Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wiki hii kinatarajia kumburuza mahakamani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumtaka afute kauli yake aliyoitoa bungeni mwezi uliopita kwamba Polisi wawapige raia wanaoleta uchokozi na kuashiria uvunjifu wa amani hapa nchini.

Mwezi uliopita Pinda katika mkutano wa Bunge la bajeti mjini Dodoma alitoa kauli ya kulitaka jeshi la Polisi nchini kuwapiga raia wanaokaidi amri halali ya jeshi hilo wakati aikijibu maswali ya Papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia, alisema taratibu zote za kisheria za kumfikisha Pinda mahakamani zimekamilika na siku yoyote wiki hii watafungua kesi.

Sungusia alisema kauli ya Pinda, imevunja katiba ibara ya 13 na kwamba lazima sheria ichukue mkondo wake kwa mkumfikisha mbele ya mahakama.

Alifafanua kuwa ibara ya 100 inayompa kinga mbunge anapotoa jambo lolote bungeni inamweka kando Pinda, kwa kuwa yeye hakuzungumza bungeni kama mbunge bali alikuwa anatoa msimamo wa serikali yake.
 Alisema kauli ya Pinda ilikuwa kali na mbaya na kwamba, walimtaka Pinda aifute siku chache baada ya kuitoa, lakini mpaka sasa amekaidi na hivyo wameamua kuchukua hatua ya kumfikisha mahakamani ili haki iweze kutendeka.

Pinda alitoa kauli hiyo nzito alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyetaka kujua kauli ya serikali juu ya vyombo vya dola kudaiwa kuwapiga raia hususani katika mikoa ya Mtwara na Arusha.

Akijibu swali hilo Pinda alisema “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu.”

 Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu,"
“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga,” alisema Pinda.
 
CHANZO ( NIPASHE - Richard Makore )