SIKU moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), kueleza kusudio lao la kumshtaki Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda
kwa madai ya kuvunja katiba ya nchi Ibara ya 13 (1), wakati wa kipindi cha
maswali na majibu bungeni mjini Dodoma, Juni 19 mwaka huu, sakata hilo sasa
limezidi kuchukua sura mpya.
Hali hiyo inatokana na Mbunge wa Tabora Mjini, Bw.
Ismail Aden Rage (CCM) kudai kuwa, hakubaliani na hauoni uhalali wowote wa LHRC
kumfikisha mahakamani Bw. Pinda ambaye analindwa na Sheria ya Haki, Kinga na
Madaraka ya Bunge namba tatu ya mwaka 1988 pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya
100.
Akizungumza na Majira Dar es
Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani
anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha
wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema,
kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki,
Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili
kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama
LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa
niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka
kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila
wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi
kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi
anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage
alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda
akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha
kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa
kumtetea na kushinda.
“Kama
leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi
mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine
kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi
kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini
lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote
wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji
huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari
juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia,
alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika
Makahama Kuu.
Alisema
Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa
usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna
nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria
sasa kama weweukijifa nyajeur iutapigwatu.
“Na
miminase mam uwapige tukwasab abu hakunana mnanyin ginemaa natumechoka ”,alise
maBw. PindaambapoB w.Sungus iaaliong eza kuwa ,kau li hiyoni kin yumech aK atiba
, S heriazanchi namising iya HakizaBinad am u.
Bw.
Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake
ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa
hajafanya hivyo.
Chanzo ( majira - Eckland Mwaffisi )
No comments:
Post a Comment